Uncategorized

Rose Ndauka Afunguka Alichojifunza Katika Ujio wa Ramsey Bongo

By  | 

Rose Ndauka Afunguka Alichojifunza Katika Ujio wa Ramsey Bongo

 

Msanii wa filamu Bongo Rose Ndauka amefunguka alichojifunza kutoka kwa Ramsey Nouah wa Nigeria katika ziara yake aliyoifanya Tanzania siku chache zilizopita.
“Nimepokea vitu vingi kwanza mabadiliko, yaani kama unahitaji mabadiliko yanaanza kwako wewe mwenyewe binafsi. Kwa hiyo nilichogundua kwamba wasanii watanzania vitu ambavyo tunalalamika hapa tatizo nini na wenzetu na wenzetu wanakutana na vitu kama hivyo wanakutana na vitu hivyo hivyo,” amesema Ndauka.
Muigizaji huyo ameongeza kwa kusema, “Lakini namna gani unataka kupiga hatua kwenda mbee hilo ndio linakuwa suala. Kwangu mimi ujio wa Ramsey Nouah kwa semina ametupatia leo nimejifunza vitu kutoka kwake na nimejifunza kuchukua Confidence yangu asilimia 100 na kuendelea kupambana na vitu vyangu nilivyokuwa navyo.”
Ramsey alikuwa na ziara nchini Tanzania wiki iliyopita na aliweza kutembelea kaburi la Marehemu Steven Kanumba pamoja na kukutana na waigizaji wa filamu nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *