Uncategorized

UTAMU WA HAMU – 3

By  | 

Related image

 

Nilisikia mtu akigonga mlango tukaacha tulichokuwa tunafanya tukajiweka vizuri kama hakuna kitu tulichokuwa tunafanya ” nenda kafungue mlango”
” sawa nilikwenda kufungua mlango huku mapigo ya moyo yakiwa yananienda mbio,nilifungua mlango huku nikiwa sijui aliyekuwa akigonga mlango nilipofungua mlango sikuamini niliyekutana nae kumbe alikuwa mwamtumu
” oooh!.. mwamtumu vipi?”
” poa tu mbona umechelewa sana?”
” aaah…kuna kazi nilikuwa namsaidia madamu Mara moja”
” mmmmh poa ushamaliza”
” ndiyo tunaweza kuondoka tu usijali” nilikuwa najibu huku kijasho kikinitoka
” sasa madamu mi naenda basis”
” haya ntakucheki baadae basis”
” sawa madm” niliondoka na mwamtumu huku nikimlaumu mwamtumu kwakuja kunialibia.
” huyu nae sijui kafata nini huku mpaka sijamkamua tena madamu…sasa na hasira zote naenda kumalizia yeye                      Ngoja”nilijisemea moyoni huku mwamtumu akiwa mbele Mimi nyuma tulielekea kwenye bustani moja ya Shule tunayotumiaga kupigia picha wakati wa maafari na likizo,basi tukaenda mpaka pale tukatafuta sehemu mzuri tukakaa sikujua mwamtumu kwanini kanileta huku kwenye bustani.
” mmmh najua utashanga sana kwanini nimekuleta huku”
” yeah nikweli sijui unachotaka kuniambia”
” najua kesho unarudi nyumbani na utaniacha Mimi huku Shule”
” najua hilo….nini point yako?”
” point yangu nikwamba nenda ila jua nakupenda sana”
” aaaah kwa ilo usijali mbona nakupenda sana”nilikuwa namwambia mwamtumu huku nikimuangalia usoni kuonesha kile nilichokuwa naongea kilikuwa kinatoka ndani ya uvungu Wa moyo Wang.
” nakupenda my love” aliniambia huku akilegwa na machozi akaninamia kifuani akawa analia.
” leo nataka nikupe zawadi usiku”
” zawadi gani?”
” utaiyona usijali”
” mmmmh…niambie basi”
” haya wewe ulitaka nikupe zawadi gain?”
” mmmh yoyote tu mpenzi wangu”
” basi ntakupa kitu ambacho hautaamini kwenye mboni za macho yako”
” mmmh…nikweli ”
” ndiyo ” alinijibu huku nikizidi kumshanga mwamtumu kwa mapenzi yake kwangu yalivyokuwa makubwa                              Tuliendelea kukaa pale huku tukipiga story za hapa na pale mpaka giza likaanza kuingia huku tukizidi kuongea mpaka tulipokuja kustuka ilikuwa imetimia saa mbili kasoro
” haaa!.. unajua muda umeenda sana”
” kwani sangapi” nilimuuliza mwamtumu
” saa mbili kasoro hii”
” we basi tuondoke” nilimwambia mwamtumu huku nikiamka tulipokuwa tumekaa kwa ajili ya kuanza kuondoka
” sasa unaenda wapi?”aliniuliza mwamtumu huku akiwa amenishika mkono.
” tuondoke we hauwoni muda umenda sana na natakiwa nijiandae kesho si unajua nina safari ya kurudi nyumbani”
” najua kuwa muda umenda ila unakumbuka nilikuadi nini?”
” ndiyo si uliniambia utanipa zawadi”
” ndiyo….ila unajua ni zawadi gani ninayotaka kukupa”
” sijui unataka kunipa nini”
” basi naomba ufumbe macho”
” nifumbe macho!!?”
” ndiyo nataka nikupe hiyo zawadi niliyokuadi”
” haya bwana ngoja nifumbe” nilimwambia huku nikifumba macho yangu.
” mmmmh mbona ujafumba vizuri macho”
” nimefumba kweli tena”
” haya ngoja mpaka nikuambie ufumbue sawa”
” haya my wangu” nilizidi kufumba macho huku nikisubili aniambie nifumbue macho.baada ya dakika tano
Nikasikia sauti
” haya fumbua”
“Poa” nilipofumbua macho………..ITAENDELEA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *