Uncategorized

Zari amjibu Mobetto ‘bora mimi changudoa mzee mwenye mafanikio’

By  | 

Baada ya Hamisa Mobetto kumtibua upya mama watoto wa Diamond, Zari The Boss Lady ikiwemo kumuita mcheza picha chafu, Zari ajibu mapigo tena.Mobetto ambaye alikuwa nchini Uganda weekend iliyopita kwaajili ya show ya Girls Power, alimtupia dongo Zari na kumuita mcheza picha za uchi.Alhamisi hii Zari ameamua kumtolea uvivu Mobetto kwa kuandika ujumbe mkali mfululizo kupitia mtandao wa snapchat.“Bora mimi changudoa mzee niliye na mafanikio na bado ananipenda kuliko kijana wa miaka 20+ mama uliyeachwa solemba mara mbili na tuzo juu #MchepukoUsioNaAKili#MweweWaMwaka,” , aliandika Zari Snapchat“Kijana, kijana kila siku kijana, kijana na             mzuri lakini huwezi kutafuta mwanaume wa kwako mwenyewe….namna chan**doa usivyojiamini, Kama unajiamini na uzuri na akili basi acha tuone mwanaume gani atakutaka baada ya drama hizi, baby daddy 3 loading ukiwa na miaka 20+ atakuwa mjinga pia,” alisema Zari kupitia ujumbe huo.Zari akaongeza “sio wewe cha***doa uliyelia social media ukidai Lulu kakuibia bwana’ko lakini umegeuka kufanya hicho hicho ulicholilia wakati unajua inavyouma, Mungu hawezi kubariki furaha yako juu ya maumivu ya mwanamke mwingine…ng’oo!!!”

 

“Unaweza kupost picha zote za nyuma ukiwa nae, lakini tayari nimekwisha msamehe makosa yake yaliyopita. Siwezi kubadilisha historia….nimechukulia kawaida naendelea kujenga maisha yangu ya kesho. Uchawi wote unaisha nguvu na sasa anarudi kwa akili zake kumrudia,” amesema Zari na kusisitiza.Baada ya madongo hayo, Mobetto bado hajatoa kauli yoyote kwenda kwa Zari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *